Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha muhandisi Andrew Lucas Ako akiongea na waandishi wa habari Katika maonyesho hayo.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco wakiwa katika banda lao lililopo Katika maonyesho ya nne ya mifuko programu uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika Katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
………………………………………………………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Shirika la Umeme Tanesco limejipanga kuhakikisha umeme unafika maeneo yote ambayo wananchi wanahitaji kwa lengo la kuendeleza uchumi wa wananchi ,mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla .
Hayo yamebainishwa na kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha muhandisi Andrew Lucas Ako wakati akiongea na waandishi wa habari Katika maonyesho ya nne ya mifuko ya programu uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika mkoani humo ambapo alisema kuwa kwa upande Arusha jiji wameweza kuunganisha umeme kwa wananchi kwa asilimia 80 , na asilimia 20 waliobaki watahakikisha wanamalizia na wanaamini katika awamu hii ya miaka mitano watamalizia asilimia zilizobaki.
Alisema kuwa katika jitiada za kuisaidia serikali kuwezesha wananchi kiuchumi shirika la umeme Tanesco litahakikisha maeneo yote ambayo wananchi wanahitaji umeme ,yanawekwa kwa bei nafuu na maeneo mengine wananchi wanawekewa umeme kwa gharama za shirika kutokana na uhitaji wa wananchi lengo likiwa ni kuhakikisha wanapata hitaji lao la msingi la kupata umeme.
Alisema kuwa shirika la umeme Tanesco lipo Katika maonyesho hayoa kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi wote wanaouthuria maonyesho haya juu ya huduma zinazotolewa na shirika hilo pamoja kuwaeleza miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na tanesco mkoa wa Arusha .
“Sasa hivi tunamiradi mikubwa na midogo ambayo tunatekeleza kama mkoa kwa bajeti ya mwaka 2020/2021 ,miradi midogo tunayotekeleza ina gharimu kihasi cha shilingi bilioni 10 kwa Arusha na hadi sasa tumeshatekeleza kwa asilimia 80 na tunaamini adi ifike mwezi wa nne tutakuwa tumekamilisha “Alisema Ako.