Afisa tawala ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina akiongea mbele ya wananchi wakati wa kugawa miti iliyotolewa na Sao Hill
Na Fredy Mgunda,Iringa.
UONGOZI wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umeupongeza wa uongozi shamba
la miti la Sao Hill kwa kuendelea kutunza mazingira kwa kutoa elimu ya utunzaji
wa mazingira na upandaji wa miti kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo hata nje
ya wilaya hiyo.
Akizungumza kwa niaba mkuu wa wilaya ya Mufindi,afisa tawala ofisi ya
mkuu wa wilaya ya Mufindi,Joseph Mchina alisema kuwa kukiwa na miti utapata
faida nyingi kama vile ukiwa na miti utapata hewa
safi,ajira,mvua,chakula,matunda,moto rutuba kwenye udogo na ukiwa na miti
utapata mazingira mazuri ya kuishi.
Alisema kuwa unapoukuta mti sehemu yeyote ile unatakiwa kuutunza na
kuuthamini kutokana na thamani yake katika maisha ya mwanadamu hutengemea miti
kwa namna yeyote ile na amewapongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS
kupitia shamba la miti la Sao Hill.
Mchina aliwaomba wananchi kuacha tabia ya kukata miti ya asili hovyo
ili kuepuka kuharibu mazingira kwa makusudi na kuleta madhara makubwa katika
maisha ya binadamu hivyo inakiwa kila mwananchi kuendelea kutoa elimu kwa kila
mtu ambaye hana elimu ya umuhimu wa miti.
“Ninaamini kuwa hakuna mtu ambaye hajui umuhimu wa misitu kwa kuwa
hakuna kiumbe chochote kile duniani ambacho hakitui misitu au miti katika
kuendesha maisha yake hivyo ni mhimu kila mtu kuhakikisha anatunza miti na
mazingira” alisema Mchina
Aidha Mchina alisema kuwa kitendo cha viongozi wa shamba la Sao Hill
kutoa miche ya miti milioni moja bure kwa wananchi wa wilaya hiyo ni kukuza
uchumi kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla kutokana na
faida za miti.
Alisema kuwa uwepo wa shamba la miti katika shamba hilo la serikali
limechangia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi wengine wa wilaya hiyo
kuanza kupanda miti na hadi hii leo bado wanapanda miti na umekuwa uchumi wa
wananchi.
Mchina alisema kuwa kitendo cha kutoa miti hilo bure kunawakumbusha
wananchi kuendelea kupanda miti kwenye mashamba yao ili kuendeleza utamaduni wa
kupanda miti ili kukuza uchumi kwa wananchi wanaolizunguka samba hilo.
“Ni vema tukaendelea kutunza miti ya asili na kuendelea kupanda miti
kwa kitaalamu kwa kufuata maelezo kutoka kwa wataalam ili kupunguza uharibu
unaosababishwa na sisi wenyewe kwani misitu ni mali na uhai vile vile” alisema
Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili
kulinda mazingira na kukuza uchumi kwa wananchi na amewapongeza viongozi wa
shamba la miti la Sao Hill kwa jitihada za kuendelea kutunza mazingira.
Nao wadau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna
wanavyonukaika na uwepo wa shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua
zinazochukuliwa hasa juu ya ulinzi wa mazingira.
Awali Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita
alisema kuwa jukumu la kila mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya
ulinzi wa Bayoanuai zilizopo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai
wote wakiwamo Binaadam huku
akitaja za kutoweka kwa bayoanuai
Mwita alieleza namna ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii
kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi
wa masitu ikiwamo ajira na ufugaji wa nyuki.
Alisema kuwa misiti imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani
ikiwepo kuwa makazi ya wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia chakula,ikolojia
ya misitu ya Sao Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya mto Ruaha Mkuu na
Ruaha Mdogo ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia umeme.
“Umeme unazalishwa katika vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere
wanategemea maji kutoka katoka hidhafi ya misitu ya Sao Hill kutokana na
utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema
Alisema upandaji wa miti unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili
ambazo zimekuwa zinasaidia katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu
mkubwa sana kwa wananchi kote ulimwenguni.
Aidha Mwita alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza
uchumi katika sekta mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.