…………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Zaidi ya wakulima 8000 wamenufaika na mikopo ya kilimo kutoka katika mradi wa mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo wadogo inayodhaminiwa na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) kea kushirikiana na taasisi nyingine za kifedha 10.
Akiongea na waandishi wa habari Katika maonesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshaji yanayoendelea mkoani Arusha Afisa mwandamizi wa benki ya maendeleo ya kilimo George Nyamrunda alisema kuwa mfuko huo ni mfuko unaratibiwa na banki hiyo kwaajili ya kuhamasisha au kuchagiza benki na taasisi nyingine za fedha ziweze kukopesha wakulima.
Alisema kuwa kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakikosa uwezeshaji kupitia mabenki wakiambiwa kuwa hawakopesheki kwasababu hawana dhamana hivyo benki hiyo kupitia mfuko huo wamekuwaja na suluhu ya kuwapatia dhamana mabenki Ili waweze kukopesha wakulima.
“Mpaka sasa tuna ushirika na tasisi za kifedha kumi ambazo tunawapatia dhamana na wao waweze kuongeza uwekezaji katika kilimo ambapo kinachofanyika ni mabenki yanakopesha wakulima alafu benki ya kilimo inatoa dhamana na wakishindwa kulipa tunafidia ile hasara ambayo mabenki yamepata,” Alisema Nyamrunda.
Alieleza wameshadhamini mikopo ya zaidi bilioni 69 kwa muda wa miaka miwili tangu kuanzishwa kea mfuko huo ambapo wameweza kuwafikia wanufaika 8500 huku asilimia 95 wakiwa ni wakulima wadogo.
Alifafanua kuwa lengo la mfuko huo ni kuhamasisha mabenki mengine kuisaidia benki ya kilimo ambayo ndio inajukumu la kuwezesha sekta ya kilimo lakini kutokana na uhitaji wa mitaji kikubwa wakahamasisha na mabenki mengine kuwekeza.
Aliendelea kusema kuwa faida kubwa waliyopata mpaka sasa ni kushusha ribya ya mikopo inayotolewa kwa wakulima kutoka Asilimia 20 hadi 24 na kufikia Asilimia 14 hadi 17.
Kwa upande wake Lucius Mtewele meneja mikopo ya kilimo kutoka benki ya TPB alisema kuwa wanategemea mashirikiano hayo Katika kuendeleza kilimo na wanaamini wataweza kuwafikia wakulima wengi zaidi na kunyanyua maisha yao.
Naye meneja mahusiano kilimo biashara kutoka benki ya CRDB kanda ya kaskazini Rogers Mselle ushirikiano huo umeweza kuwasaidia kuwafulikia wakulima wengi zaidi na kuweza kuwafikia wakulima na kutoa mkopo zaidi ya bilioni 15 kupitia dhama iliyotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo na kufikia wanufaika 1200.
Picha
1. picha ikionyesha Afisa mwandamizi wa benki ya maendeleo ya kilimo George Nyamrunda akiongea na waandishi wa habari katika maonyesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika Katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha