************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya ugunduzi wa fuvu la zinjanthropus tarehe 22 julai mwaka huu na miaka 60 ya hifadhi ya Serengeti.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo Prof. Audax Mabula amesema kuwa sherehe za awali ambazo zilikuwa zifanyike julai 17 sasa zitafanyika julai 22 mwaka huu eneo la Olduvai ndani ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Amesema kuwa pia kuna mabadiliko ya warsha iliyokuwa inaandaliwa kufanyika Tarehe 16 julai sasa itafanyika tarehe 20 julai mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.
“Kutoka na sababu zisiweza kuzuilika sherehe za ugunduzi wa fuvu la kale ambazo zilikuwa zifanyike julai 17 sasa zitafanyika Julai 22 eneo la Olduvai na Mh.Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo hivyo wananchi wote mnakaribishwa kuja kujionea fuvu la mwanadamu wa kale siku hiyo”
Amesema kuwa kutakuwa na ofa maalumu ya kutembelea makumbusho ya olduvai pamoja na maonyesho maalumu kutoka sehemu mbali mbali nchini yenye urithi wa kiutamaduni yataendelea kama yalivyopangwa kuanzia tarehe 17 hadi 22 juali mwaka huu.
Ameeleza kuwa Kutokana na maadhimisho hayo watafiti kutoka sehemu mbali mbali duniani wanatarajiwa kukutana jijini Arusha kuanzia julai 17 na watalii wakiwamo wa ndani wanatarajiwa kutembelea maeneo hayo ambapo fuvu hilo kwa Mara ya kwanza litatolewa hadharani na kuonyeshwa ambapo watu mbalimbalinwatapata fursa ya kujionea.
Amesema kuwa kauli mbiu ya siku hiyo “Tujivunie urithi na chimbuko letu” ambapo aliwataka wananchi wote kpenda kutembelea hifadhi hiyo ya Ngorongoro kujionea maajabu ya binadamu wa kale na kuweza kuutangaza utalii wa ndani.
Alisema kuwa ili kuhamasisha Watazania na watalii kufuatilia maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Olduvai na Serengeti taarifa zinapatikana kwenye mitandao kwa anuani #Tanzaniazinjanthropus60years na #tanapa@60.
Ugunduzi w zinjanthropus katika tafiti za chimbuko la mwanadamu wa kale pamoja na fuvu ni moja ya rasilimali za kutangazwa kote ulimwenguni na siku hiyo kwa mara ya kwanza fuvu hilo litawekwa Olduvai Gorge ni faida yetu kiuchumi na kiutalii.