Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Dk.Abel Nyamahanga kulia akimkabidhi mifuko ya saruji mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo , Kilian Myenzi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Dk. Abel Nyamahanga akizungumza wakati alipotembelea eneo linalojengwa ofisi ya CCM wilaya ya kilolo
Mbunge wa Jimbo la Kilolo , Justin Nyamoga akizungumza
Baadhi ya madiwani wakifatilia kikao Cha maadhimisho ya miaka 44 ya CCM.
………………………………………………………………………………
NA DENIS MLOWE,IRINGA
CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Iringa katika kusheherekea miaka 44 ya kuzaliwa kwake kimetoa jumla ya mifuko 200 ya saruji na tani 15 za kokoto kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya wilaya ya CCM wilaya ya Kilolo inayotarajia kujengwa wilayani huko kwa gharama ya shilingi million 268.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Dk. Abel Nyamahanga alisema kuwa ujenzi huo uanze kwa haraka na wanatarajia hadi kufika Machi mosi watakapotembelea jengo liwe limefika hatua nzuri.
Alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa na CCM mkoa kwa lengo la kuharakisha ofisi ya CCM wilaya Kilolo kwa kuwa ndio wilaya pekee ambayo ilikuwa haina ofisi Zaidi ya kutumia ofisi ya tawi kama ofisi ya CCM wilaya.
Alisema kuwa chama hicho kimekuwa kikifanya shughuli zake kwa uhakika hivyo ni muhimu kwa kila wilaya kuwa na ofisi ambazo ni za kisasa hivyo ujenzi wa ofisi hiyo uarakishwe na ifikapo march 1 2021 ofisi ianze kutumika.
Nyamahanga alisema kuwa wanachama kuacha uoga na kusimama imara katika kuikumbusha serikali kukumbusha waibu wake kwa wananchi waliowachagua
Alisema ni sahihi kiongozi na mwanachama kuwa na shughuli zake binafsi kwa kujishughulisha kwa kujishughulisha katika shughuli mbalimbali ili kuendelea kutunza familia ili kuondokana na utegemezi uliopo baina ya watu
Alisema milango isifungwe kusikiliza kero za wananchi kwani wananchi wengi wamekuwa wakitegemea chama cha mapinduzi na kuacha kuvaa gwanda wakatika wa uchaguzi ili kuendelea kuweka uaminifu kwa wananchi bila kujali kipindi chake
“tusifunge milango ndugu zangu imekuwa ni tabia ya watu wengi wakipata changamoto sehemu ya kwanza ni chama cha mapinduzi kwani ndiko ulipo msaada tuache tabia ya kuvaa gwanda kipindi cha uchaguzi tuvae wakati wote ili kuondoa ile tabia ya kusema hawa ccm watafungua mlango kipindi cha uchaguzi “ alisema
Aliwataka viongozi kutafakari ushirikiano na mshikamano uliopo baina ya viongozi kwa hakuna sababu ya kuweka utofauti kwani inajengwa nyumba iliyomoja kwa kuboresha mshikamano baina ya chama na watumishi wa serikali ili kuijenga nchi iliyo moja.
“hakuna sababu ya kuweka utofauti kiu yetu kuendelea kushikamana na kuendelea kuzungumza kitu kimoj ni Dhahiri wakati wote viongozi wa chama ndani ya miaka 44 kutafakari chama kimekuwa kwa kinachostahili hivyo hatua ipi uongozi wetu ni wa aina ipi kuwanyenyekea walionichagua au nafanya yanayostahili” alisema
Alisema wananchi wanatakiwa kutumikiwa kwani aibu ya kiongozi ni aibu ya chama cha mapinduzi na kuacha tabia ya mazoea katika utendaji hivyo kuwatumikia wananchi kwa kufuata kila hatua bila kutenga wala malumbano.
Aidha katibu wa Ccm mkoa wa Iringa,Brown Mwangomale aliwashauri madiwani wa halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Aliongeza kuwa wahakikishe wanafanya kazi za wananchi kama walivyoomba kuwatumikia ili kuendelea kuweka uaminifu kwa wananchi kwani bila kufanya hivyo itawia ugumu kwa mwaka 2025 katika uchaguzi.
Daudi Yassin ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi alisema kuwa viongozi waliochaguliwa wanatakiwa kushiriki katika kutatua changamoto za wananchi kwa vitendo huku wakionyesha mambo azuri yaliyofanywa na chama chama cha mapinduzi kwa miaka 44
Aidha Christian Nyamoga ambaye ni mbunge wa Kilolo amesema kuwa anapongeza ushindi wa Chama cha Mapinduzi kutokana na mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Magufuli na hivyo kufanya Nchi ya Tanzania kuwa tofauti na miaka iliyopita .
Alisema kutokana na shughuli ya ujenzi wa ofisi ya chama cha Mapinduzi wilaya ya Kilolo watashirikiana kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na ofisi kuweza kutumika.
Pia mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu alisema kuwa kama wabunge wa mkoa wa Iringa wamejipanga kuhakikisha wanashughulikia changamoto mbalimbali zilizopo huku wakizitolea ufafanuzi changamoto za wananchi wawapo bungeni huku zikitolewa dolla million 150 kwa ajili ya kuendeleza utalii.
Killian Myenzi ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Kilolo alisema kuwa matatizo ya uongozi ni moja ya sababu zilizopelekea ucheleweshwaji ujenzi wa ofisi ya wilaya hivyo kama kiongozi atatekeleza wajibu wake kusimamia ujenzi bila kuwa na ubadhirifu wowote
“matatizo ya uongozi ni moja ya changamoto kwa sababu kila kiongozi anataka atoe mawazo yake hivyo kutokana na mawazo hayo yamepelekea tuchelewe ni aibu sana miaka 20 ofisi hakuna lakini napenda niseme nimejipanga sitaruhusu haya moja ya kokoto kutumika katika manati nitahakikisha hakuna kinachoharibika .
Alisema vijana wanahitajika kuwa imara na kukosoa mahala ambapo kuna baadhi ya mambo hayakwendi vizuri ili kuendelea kuweka uaminifu pia kuwatatulia wananchi changamoto zinazowakabili katika jamii.