MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene Wilayani Mpwapwa mara ya kuitembelea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akishiriki katika zoezi la kujimba Msingi kuashiri kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene Wilayani Mpwapwa mara ya kuitembelea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafene Kata ya Lumuma wilayani Mpwapwa mara baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene mara ya kuitembelea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akiwahimiza wananchi wa kijiji cha Mafene Kata ya Lumuma wilayani Mpwapwa kuwekeza nguvu katika ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ili ndani ya mwezi wa ianze kutumika mara ya kufanya ziar ya kuitembelea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Lumuma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,wakati akitoa hotuba mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Katibu wa CCM Wilaya ya Mpwapwa Sophia Kiwanga,akielezea walivyojipanga kukamilisha ujenzi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ili iwe kukamilika kwa wakati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lumuma,akitoa wito kwa wananchi wa Mafene wilayani Mpwapwa kushikamana ili waweze kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ili watoto wao waanze kusoma kuanzia mwezi wa Marchi mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Mwenyekiti CCM Wilaya ya Mpwapwa George Chigwile,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafene Kata ya Lumuma wilayani Mpwapwa walioshiriki zoezi la kujimba msingi wa Madarasa ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Henry Msunga,akitoa neno kwa wananchi wa kijiji cha Mafene Kata ya Lumuma wilayani Mpwapwa mara baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Mtendaji Kata ya Lumuma Bi.Oliver Ipyana,akitoa taarifa ya ujenzi kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa (hayupo pichani) ambaye alifanya ziara ya kukagua na kujionea ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Katibu CCM Kata ya Lumuma Paul Kibawa,akitoa taarifa ya chama katika Kata hiyo tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu pamoja na Mikakati ya kukamilisha kwa wakati ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bw.Paul Sweya,akimuelezea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa (hayupo pichani) kuhusu alivyojipanga kuhakikisha wanafunzi wote ndani ya Wilaya hiyo watajiunga na masomo na kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene kwa wakati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
Diwani wa Kata ya Lumuma Joctan Cheliga,akizungumza jinsi walivyojipanga na wananchi wa Kata yake kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene ili wanafunzi waweze kujinga na masomo kwa wakati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM leo Februari 2,2021
………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Mpwapwa
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Mafene huku akiagiza ujenzi huo ukamilike kabla ya Machi mwaka huu.
Mkanwa ameto maagizo hayo leo Februari 2,2021 Wilayani Mpwapwa mara baada ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma walipotembelea ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.
Mkanwa amesema kuwa nataka ujenzi wa Shule hii ukamilike kabla ya Machi mwaka huu ili wanafunzi 188 waliokosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza waanze masomo haraka.
”Nataka ujenzi huu ufanyike usiku na mchana ili ukamilike kwa wakati huku akiagiza utaratibu wa wananchi kuchangia kwa awamu ujenzi wa shule hiyo ya sekondari ya kata ambao ni sh. 20,000 kwa kwa kaya unapaswa kufanyika kwa mara moja ili kuwawezesha wanafunzi hao kuanza masomo kama ambavyo serikali ilivyoagiza”amesema Mkanwa
Mkanwa amesema kuwa Madarasa ndio yanapaswa yasubiri wanafunzi na sio wanafunzi kusubiri madarasa. Kwa mipango mliyoweka wanafunzi hawatoweza kuanza masomo Machi mwaka huu.
Katika kuunga mkono jitihada za ujenzi wa shule hiyo, mwenyekiti huyo ameahidi kuwa CCM Mkoa wa Dodoma itachangia mifuko ya saruji 100 ambapo Jumamosi atakabidhiwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa, Jabiri Shekimweli.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mpwawa, Paul Sweya, amesema kuwa halmashauri itahakikisha ujenzi huo unakamilika kabla ya Machi mwaka huu kuwawezesha wanafunzi hao kuanza masomo.
Bw.Sweya amesema kuwa baadhi ya vifaa vya ujenzi halmashauri inavyo, hivyo wananchi wakikamilisha kujenga maboma, halmashauri itawaunga mkono.
Awali Mtendaji wa Kata ya Lumoma, Oliva Ipyana, amesema kuwa wananchi wameanza ujenzi wa shule hiyo kwa kuchimba msingi tayari kujenga madarasa manne, ofisi ya walimu na matundu sita ya vyoo kwa makadirio ya sh. milioni 30.
Bi.Ipyana amesema kuwa walifanya mchanganuo kubaini idadi ya watu wanaopaswa kuchangia ujenzi huo ambapo kwa Kijiji cha Mafene watachanga wananchi 800 kiasi sh. milioni 16, Kijiji cha Kitati watachangia watu 400, sh. milioni 8 huku wananchi 270 wa Kijiji cha Lufusi watachangia sh. milioni 5.4.
Amesema kuwa katika kufanikisha ujenzi huu, Kijiji cha Mafene kimetoa hekari 60 za kujenga shule hiyo ya kata.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Henry Msunga, amesema kuwa maadhimisho ya miaka 44 tangu kuasisiwa kwa chama hicho kikongwe Afrika, mwaka huu yanafanyika kwa kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo zilizofanywa na wananchi kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo ambao ndio makao makuu ya chama na serikali.