*****************************************
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa,Justin Nyamoga amezipongeza kampuni ya New Forest, shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa kwa kufanikisha ujenzi la bweni la shule sekondari Mazombe.
Ujenzi huo umejengwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Lugalo wilaya ya Kilolo kwa ajili ya wasichana wa Shule ya sekondari Mazombe waliokuwa wakipata changamoto ya baadhi kukosa makazi na kupanga uraini.
Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi na kuwashukuru kwa kukichagua chama Cha Mapinduzi kwa kura nyingi na kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo Hilo, Nyamoga alisema moja ya ahadi zake kuhakikisha sekta ya Elimu inakuwa Katika Jimbo la Kilolo.
Alisema kitendo cha kampuni ya Forest na Lyra in Africa ni Cha kuungwa mkono kwani inaonyesha ni kiasi gani wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Aidha Nyamoga aliwashukuru wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo na wananchi wa kijiji cha Mazombe kwa ushirikiano wao mzuri wa kujenga bweni la wasichana katika shule sekondari ya Mazombe kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa utoro na mimba zisizotarajiwa.
Akizungumzia tatizo Ia maji katika Kata hiyo Nyamoga alisema kuwa litatatuliwa kwasababu serikali inatekeleza mradi mkubwa wa maji unaogharimu takribahi shilingi Bilioni 10 za Kitanzania kwa ajili ya kutatua kero hiyo kwa wakazi wa kata ya Lugalo.
Aidha alisema kuwa ataendelea kushirikiana nao ili kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mbigili na kufanya ukarabati wa shule ya msingi Mbigili.
Katika Ziara hiyo Nyamoga alitembelea shule ya msingi Mkawaganga shule ya msingi Mbigili. zahanati ya Mazombe na zahanati ya Mbigili kwa lengo la kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo kuweza kuzitatua kwa kushirikiana na wananchi na serikali kwa ujumla.