Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Jerry Mwaga akijibu hoja mbalimbali za Madiwani jana .
……………………………………………………………………………………………
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imeanza mpango wa kuwekea mawe ya utambuzi wa eneo la mipaka ya makumbusho ya Mtemi Milambo kwa ajili ya kulilinda kisheria ili lisiweze kuvamiwa na kupoteza histoaria yake.
Hatua hiyo inalengo la kuhakikisha kuwa eneo hilo lenye Historia kubwa hapa nchini linaendelea kuwa endelevu kwa ajili ya manufaa ya wakazi wa Kaliua na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri hiyo Jerry Mwaga wakati Baraza la Madiwani alipokuwa akijibu hoja ya Madiwani waliotaka maeneo yote ya vivuto vya Kihistoria na utalii kutunzwa kwa ajili ya kuongeza mapato ya ndani na Taifa kwa ujumla
Alisema mbalimbali na eneo hilo wataendelea kuainisha maeneo yote ya kale na yenye vivutio kupitia vigezo vinavyotakiwa ili yaweze kutambuliwa na kulinda kisheria kwa lengo la kuwavutia watalii wa ndani na nje.
Diwani wa Kata ya Usimba Benjamin Masanja alishauri kuwa maeneo ya kihistoria yaliyopo wilayani Kaliua yanatakiwa kuboreshwa na kuweka watu wanaoweza kuelezea kwa ufasaha historia ya eneo husika kwa ajili ya kuwavutia watu mbalimbali wanaofanya utafiti na wale watalii kuyatembelea.
Alisema hatua hii itaiwezesha Halmashauri kupata mapato na baadhi ya wananchi kupata ajira ya kuongoza Watalii na watafiti watakaopenda kujifunza kuhusu utajiri wa historia ya mambo ya kale yaliyopo wilayani humo.
Naye Diwani wa Kata ya Kazaroho Haruna Kasele alishauri kuwa wakati umefika kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ikaanza kuwekeza katika maeneo ya historia za kale ili kuvutia watalii wengi kutembelea maeneo husika.
Alisema hatua itawezesha Halmashauri hiyo kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya ndani na kupata fedha kwa ajili ya kupeleka huduma za kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo utoaji wa huduma za afya , elimu na zile za ugani.
Kasele alisema Halmashauri ikiwekeza fedha kuboresha Makumbusho ya Mtemi Milambo, eneo la kunyongea watumwa ambalo lilikuwa maarufu kwa jina la Iselamagazi na njia ya Wajerumani ambayo inaanzia Ndorobo wilayani Urambo kupitia Kazaroho wilayani Kaliua wataongeza mapato ya ndani.