WINGA Mghana, Bernard Morrison ametokea benchi na kufunga mabao mawili Simba SC ikiibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Simba Super Cup jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Morrison aliingia kuchukua nafasi ya kiungo Mkenya, Francis Kahata kabla ya kufunga mabao mazuri dakika za 87 na 90 na kwenda kushangilia kwa kuweka mpira ndani ya bukuta yake kwa mbele kuwabeza waliosema yeye ni mgonjwa wa ngiri.
Na Morrison aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC tangu asajiliwe kutoka kwa mahasimu, Yanga Agosti mwaka huu alifunga mabao hayo baada ya viungo wengine wa kigeni, Mzambia Larry Bwalya na Mzimbabwe Perfect Chikwende kutangulia kufunga.

Bwalya aliyetua Simba SC Agosti kutoka Power Dynamos ya kwao, Zambia alifunga bao la kwanza dakika ya 39 na Chikwende aliyejiunga na Wekundu hao wa Msimbazi mwezi huu kutoka FC Platinums ya kwao, Bulawayo akafunga la pili dakika ya 72.
Michuano hiyo itaendelea keshokutwa kwa mchezo kati ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Al Hilal, kabla ya kuhitimishwa Jumapili kwa mchezo kati ya Simba na Mazembe.