Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akiwaongoza viongozi wa wataasisi mbalimbali na watumishi wa halmashuri ya jiji la Dodoma katika zoezi la kupanda miti pembezoni mwa barabara katika kata ya Mkonze jiji Dodoma leo Januari 23,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akiangalia ubovu wa barabara ya dhambi iliyopo Kata ya Mkonze Mkoani Dodoma huku akitoa siku tano kwa TARURA kufanya marekebisho ili wananchi waweze kupita leo Januari 23,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akimtazama bodaboda akipita katika barabara iliyoharibiwa na Mvua alipokuwa akiwaongoza viongozi wa wataasisi mbalimbali na watumishi wa halmashuri ya jiji la Dodoma katika zoezi la kupanda miti pembezoni mwa barabara katika kata ya Mkonze jiji Dodoma leo Januari 23,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza na viongozi wa wataasisi mbalimbali na watumishi wa halmashuri ya jiji la Dodoma mara baada ya kuwaongoza katika zoezi la kupanda miti pembezoni mwa barabara katika kata ya Mkonze jiji Dodoma leo Januari 23,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akitoa maagizo kwa TARURA ndani ya siku tano wawe wamefanya marekebisho katika barabara ya dhambi iliyopo Kata ya Mkonze jijini Dodoma leo Januari 23,2021.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru,akielezea jinsi jiji walivyojipanga katika muendelezo wa kupanda miti katika jiji hilo leo Januari 23,2021.
Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro,akitoa taarifa jinsi hali inavyoendelea katika upandaji wa miti mara baada ya kupanda miti pembezoni mwa barabara katika kata ya Mkonze jiji Dodoma leo Januari 23,2021.
…………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amewataka viongozi wa halmashauri za Mkoa wa Dodoma kujenga utaratibu wa kutembelea na kufuatilia maeneo yote yanayopandwa miti kuona kama miti hiyo inahudumiwa ili kuweza kuona matokeo mazuri ya zoezi hilo.
Dkt Mahenge ametoa wito huo wakati wa zoezi la kupanda miti pembezoni mwa bara bara katika kata ya Mkonze jiji Dodoma, amesema zoezi hilo ambalo mwitikio wake umekuwa mzuri lakini kama ufuatiliaji hautafanywa hakutakuwa na matokeo yaliyotarajiwa.
“Zoezi hili ni zuri sana lakini kama hatufanyi ufuatiliaji zoezi hili halina maana hakikisheni mnafuatilia maeneo yote yaliyopandwa miti ili kuona namna inavyoendelea” amesema Dkt Mahenge.
Aidha amefurahushwa na kitendo cha wakazi wa mitaa ya kata ya Mkonze kwa kujitoa katika zoezi la kupanda miti na kuunda kamati ya kufuatilia miti hiyo na kuahidi kuwachangia shilingi laki tano katika kamati hiyo.
“Nimesikia mmeunda umoja wenu kwa ajili ya kufuatilia miti iliyopandwa ni jambo zuri sana na la mfano, na mimi nitawachangia laki tano katika umoja wenu” amesema.
Amesema Serikali inawekeza miradi mingi sana katika jiji la Dodoma sasa ni wajibu wa wananchi kupanda miti kwa wingi ili kupendezesha jiji la Dodoma na sio kuacha eneo yakiwa makame yakipandwa miti jiji litapendeza sana.
Aidha akiwa katika eneo hilo amebaini kuwepo na korongo ambalo limekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo linalosababisha usumbufu hasa kipindi cha mvua kwa watumiaji wa vyombo vya moto.
Ametoa siku tano kwa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Mkoa wa Dodoma kurekebisha tatizo hilo na eneo lipitike na wananchi hao.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu wa jiji la Dodoma bwana Dickson Kimaro amesema katika eneo hilo imepandwa miti elfu mbili (2000) huku zoezi kama hilo likiendelea katika shule ya msingi Ipala na katika shule zote.
Nae mwenyekiti wa mtaa wa Miganga Bw.Ludovick Chogwe amepongeza utaratibu wa Mkuu wa Mkoa na viongozi wa halmashauri kuendesha zoezi la kuhamasisha wananchi kupanda miti na kusema hilo linaamsha mwitikio mwa wananchi kuendelea kupanda miti.