**********************************************
KATIKA mkutano wa Klabu ya Simba SC na waandishi wa habari unaoendelea muda huu katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam, miongoni mwa mambo yaliyowekwa wazi ni pamoja na ujio wa michuano maalum ya kujipima nguvu kwa ajili ya mechi za Klabu Bingwa Afrika (CCL).
“”Tunatangaza mashindano mapya ya SIMBA INTER CUP ambayo yatashirikisha timu tatu. Simba SC, TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan. Mashindano yataanza Januari 27 hadi 31, 2021.
“Mashindano hayo ni maandalizi ya ligi ya mabingwa Afrika na yataanza Jumatano ijayo saa 11:00 jioni na yatashirikisha timu hizo mbili pamoja na Simba wenyewe ambao ni wenyeji,” amesema Barbara.
Uzunduzi rasmi wa SIMBA SUPER CUP 2021
Naye Afisa Habari wa Klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa kupitia mashindano hayo Wanasimba watapata nafasi ya kuwaona wachezaji wapya na kocha.
“Kuanzia kesho tutatangaza watu ambao tumewaongeza katika benchi la ufundi,” amesema Manara
Kuhusu suala la Kocha Mkuu na benchi la ufundi kwa ujumla, Manara amesema “Kocha mkuu tutamtambulisha ndani ya siku mbili zijazo kama atakuwa Ibenge, Micho au mwingine yoyote tutamuweka hadharani. Lakini kuanzia kesho tutawaja makocha wawili wasaidizi watakao ungana na Suleiman Matola,”.