Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo 21/01/2021 amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokwenda kujitambulisha rasmi kwa Mhe. Rais ambapo Rais Dkt. Mwinyi amelipongeza Jeshi hilo kwa utendaji kazi mzuri. Picha na Jeshi la Polisi