Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiongoza kikao cha kamati hiyo na Watendaji Wakuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, walioongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha maelezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Muundo na Majukumu ya Ofisi hiyo, Sera, Uratibu na Bunge pamoja na Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu mbele ya Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo kwenye picha) akiwasilisha maelezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Muundo na Majukumu ya Ofisi hiyo, Sera, Uratibu na Bunge pamoja na Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)