Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa na Dk. Richard Mhangwa wakati akifanya ziara ya kukagua Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI linalotekeleza Afua za kupambana na VVU na UKIMWI kwa Watoto na familia zao Dk. Sekela Mwakyusa, ametembelea kuona utendaji kazi katika Kliniki ya Tiba na Matunzo (CTC) ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Dk. Sekela amefanya ziara hiyo leo Jumatano Januari 20,2021 akiwa ameambatana na baadhi ya maofisa wa Shirika hilo la AGPAHI, ambapo ameeleza kuridhishwa na utoaji wa huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Alisema baada ya kutembelea Kliniki hiyo na kuuliza maswali na kujionea utendaji kazi, amefarijika kuona ubora wa huduma ambazo zinatolewa kwa WAVIU.
“Niwapongeze sana watumishi ambao mnatoa huduma kwenye Kliniki hii ya Tiba na Matunzo kwa watu ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kwani mnafanya kazi nzuri sana,” alisema Dk. Sekela.
“Pale ambapo kuna changamoto msisite kutuambia, ili tuitatue hasa katika kipindi hiki ambapo tunaelekea ukingoni mwa kufunga mradi wetu,” aliongeza Dk. Sekela.
Naye Kiongozi wa Kliniki ya Utoaji wa Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dk. Richard Mhangwa amelipongeza Shirika hilo la AGPAHI, kwa mchango wao katika kusaidia utoaji wa huduma kwenye Kliniki hiyo.
Akiwa mkoani Shinyanga, Dk. Sekela pia Januari 19,2021 alishiriki kikao kazi cha kutathmini mradi wa Boresha kwa mwaka wa nne ukishirikisha Shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI linalotekeleza Afua za kupambana na VVU na UKIMWI kwa watoto na familia zao na serikali mkoa wa Shinyanga
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kaimu Katibu Tawala Mkoa ambae ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa,Mganga Mkuu wa Mkoa,Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na Wilaya,Wajumbe wa Timu za Usimamizi na Uendeshaji Huduma za Afya Mkoa na Halmashauri na Watendaji wawakilishi Idara ya Uhasibu ngazi ya Mkoa na Halmashauri.
Dk. Sekela alisema lengo la mradi wa Boresha ni kuimarisha Ufuasi na Ubakizaji wa WAVIU kwenye huduma za Tiba na Matunzo,Kuhakikisha ubora na matumizi sahihi ya takwimu za VVU na UKIMWI katika ngazi mbalimbali za maamuzi, kuendelea kuimarisha utekelezaji wa huduma unganishi zikiwemo za Kifua kikuu, Afya ya Uzazi na Mtoto, Huduma za Maabara na Famasia pamoja na Saratani ya mlango wa kizazi sambamba na Huduma za kuzuia unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto
“AGPAHI kwa kushirikina na Serikali ya mkoa wa Shinyanga, tumeendesha kikao cha kujadili tathmini juu ya mradi wetu wa Boresha kwa mwaka wa nne, ambao tunautekeleza hapa mkoani Shinyanga, wa kutoa huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi ya Ukimwi (VVU), pamoja na kuzuia maambukizi mapya, ili tunapoelekea kwenye mwaka wa tano wa utekelezaji, tuutekeleze vizuri na kusiwepo na changamoto zilizojitokeza huko nyuma,”alisema Dk. Sekela.
Kwa upande wake ,Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa mkoani Shinyanga Alphonce Kasanyi, akimwakilisha Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, aliwataka watalaamu hao wa afya, washirikiane kikamilifu na maofisa kutoka Shirika la AGPAHI,na kutatua changamoto zilizojitokeza kwa awamu zilizopita, ili mradi huo wa Boresha utekelezwe vizuri na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, akizungumza na watumishi wa Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Januari 20,2021.
Meneja mradi kutoka Shirika la AGPAHI Mkoani Shinyanga Dk. Adarick Makome akizungumza kwenye Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu wanaoishi na Maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Dk. Richard Mhangwa kutoka Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, mara baada ya Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa alipotembelea kwenye Kliniki hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa kwenye Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, akifuatilia utoaji wa huduma kwa watu hao.
Baadhi ya watoa huduma wa Kliniki ya Tiba na Matunzo ya watu ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, wakiwa na baadhi ya watumishi wa Shirika la AGPAHI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kulia akiteta jambo na washauri wa huduma ya VVU katika kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kulia, akimsikiliza Mshauri wa VVU Paulo Seleman katika Cliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa na Dk, Richard Mhangwa wa Kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga, wakati wa ziara ya kukagua utoaji wa huduma kwenye Kliniki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, kushoto, akiwa na Dk. Richard Mhangwa wa Kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga, kulia, wakati wa ziara ya kukagua utoaji wa huduma kwenye Kliniki hiyo, katikati ni Meneja mradi wa Shirika la AGPAHI Mkoani Shinyanga Dk. Adarick Makome.
Mkurugenzi wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, (wa tatu kutoka kushoto), wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukagua Kliniki ya Tiba na Matunzo katika Hospitali ya Rufa ya Mkoa wa Shinyanga, ambayo inatoa huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Januari 19,2021 : Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa mkoani Shinyanga Alphonce Kasanyi, akimwakilisha katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela akieleza namna shirika la AGPAHI linavyosaidia katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile akizungumza kwenye kikao cha kutathmini mradi wa Boresha kwa mwaka wa nne uliohudhuriwa na baadhi ya watumishi wa afya, Waganga wakuu wa wilaya na waratibu wa Ukimwi, ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa mkoani Shinyanga Alphonce Kasanyi, akimwakilisha katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela.
Meneja mradi wa Shirika la AGPAHI Mkoa wa Shinyanga Dk. Adarick Makome, akizungumza kwenye kikao hicho wakati akiwasilisha mada.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la AGPAHI Dk. Sekela Mwakyusa, wa kwanza kushoto, akiwa na washiriki kwenye kikao hicho wakisikiliza uwasilishwaji wa mada juu ya mradi wa Boresha.
Washiriki wakiwa kwenye kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Elias Masumbuko, Mfamasia kutoka Wilaya ya Kahama, akichangia kwenye kikao hicho.
Dk. Philibert Ng’wenda Mratibu wa kifua kikuu na ukoma Wilayani Kishapu, akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Dk. Henry Sylivester, Mratibu wa kudhibiti Ukimwi kutoka Kahama Mji, akichangia kwenye kikao hicho.
Na Marco Maduhu-Shinyanga.