***********************************************
Na Woinde Shizza ,ARUSHA
waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Sindile ameridhishwa na ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mfano nchini ya Patandi maalum iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru.
Haya yamejiri wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotelelezwa kwa Mpango wa Lipa kutokana na Matokeo (EP4R) katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo amepongeza ujenzi wa shule ya Sekondari ya Patandi maalum iliyogharimu zaidi ya Bilioni 3.
Silinde ameeleza kuwa Serikali mbali na kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia mpango wa EP4R imeweka mikakati ya kuendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kwa kuanza ujenzi wa shule za Sekondari 1000 .
Aidha, Silinde amesema ujenzi wa shule hizo 1000 utafanyika kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza shule 154 zitajengwa.
Silinde amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa usimamizi wa miradi Wilayani humo sambamba na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Meru na Arusha kwa ubunifu na utendaji kazi wenye tija katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa na utekelezaji wa Miradi ya P4R .
Naye Dkt.John D. Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru la Mashariki ameishukuru Serikali kwa kuongeza thamani ya Jimbo la Arumeru Mashariki kwa ujenzi wa shule hiyo.
Aidha, katika utatuzi wa changamoto za upatikanaji wa maji, kuongeza miundombinu ya taka, Nyumba za Walimu na Genereta zilizowasilishwa na Mwl.Janeth Mollel ambaye ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Patandi Maalum, Silinde ameeleza kuwa Serikali imelipokea na itatoa fedha mapema .
Katika ziara hiyo Waziri alikagua pia ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya Sekondari Sing’isi vilivyojengwa kupitia Programu ya EP4R