Afisa uhusiano mradi wa Viungo Zanzibar Muhammed Khamis akizungumza na wananchi wa Shehia ya Mtende mkoa wa kusini Unguja wakati wa utowaji wa elimu juu ya kilimo bora kupitia mradi huo ambao umefadhiliwa na umoja wa Ulaya (EU)
Baadhi ya wananchi wa shehia ya Mtende Mkoa wa kusini Unguja wakifuatilia kwa umakini mkutano wa utowaji wa elimu kuhusu mradi wa Viungo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa utowaji wa elimu kupitia mradi wa Viungo wakiwa katika picha ya pamoja.
*********************************************
Wananchi wa shehia mbali mbali za Mkoa wa Kusini Unguja wamesema ujio wa mradi wa Viungo katika shehia zao wanaamini utakwenda kubadili mfumo mzima wa maisha na wao kuwa sehemu ya jamii wenye kujiweza kiuchumi.
Waliyasema hayo mara baada ya kupatiwa elimu dhidi ya mradi wa viungo ambao utakwenda kuwawezesha wakulima kiuchumi sambamba na kulima kilimo bora.
Miongoni mwa wananchi hao Semeni Hamada Simai kutoka shehia ya Mtende alisema wameupokea mradi huo kwa mikono miwili wakiwa na mategemeo makubwa ya kufanikiwa kiuchumi.
Alisema kwa kipindi cha muda mredu wamekua wakijishughulisha na kilimo lakini kwa bahati mbaya hadi leo hii bado kilimo hakijawanufaisha inavostahiki.
Alisema kupitia mradi huo kutokana na elimu waliopewa anaamini wananchi wa mkoa huo watabadili mfumo mzima wa kilimo chao na kulima kilimo chenye tija kutoka kilimo walichozoea.
‘’Kwa miaka mingi tumekua tukijihusisha na kilimo cha mboga mboga lakini tunashindwa pakuzipeleka badala yake mboga hizo hubaki na kukopeshana wenyewe’’aliongezea.
Akibainisha baadhi ya chanagamoto ni pamoja na uhaba wa masoko ya bidhaa mbali mbali zinazozalishwa na wakulima na ndio maana wapo baadhi ya wakulima wamekua wakifanya shughuli hizo kama sehemu tu ya utamaduni wao lakini sio kupata faida.
Kwa upande wake Sheha ya Shehia ya Mtendi Khamis Ramadhani Mbara alisema ujio wa huo katika shehia hio ni jambo la faraja kubwa kwa wananchi wa kijiji chake.
Alieleza kuwa wananchi walio wengi wanahitaji kuinua maisha yao kupitia sekta ya kilimo lakini hukosa taaluma husika kutoka kwa watalaamu hubaki kuwa wakulima wa mazoea tu.
Akitoa elimu kwa wananchi hao Afisa Uhusiano katika mradu huo Muhammed Khamis alisema mradi wa viungo ni wa miaka mine uliofadhiliwa na umoja wa Ulaya (EU) wenye lengo la kuwasaidia wakumia 21,000 kutoka shehia 52 Unguja na Pemba na unatekelezwa na Jukwaa linalosaidia maendeleo ya watu Tanzania (PDF) taasisi inayojihusisha na utunzania wa misitu Pemba (CFP) pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake TAMWA-ZNZ.
Alisema kupitia mradi huo wanaufaika watapatiwa elimu ya kilimo bora kinachoendana na mahitaji ya soko la ndani nan je ya Nchi.
Alieleza kuwa kwa muda mrefu wakulima wengi Zanzibar wamekua wakijihusisha na kilimo lakini utafiti unaonesha kuwa jitihada za wakulima walio wengi bado hazijafikia melengo yao ikiwemo kuwa wakulima wenye kujitegemea na kuwa wenye kipato kikubwa.
Alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima hao ni pamoja na soko la bidhaa zao kukamatwa kwa kiasi kikubwa na madalali na kuwafanya wao kutokujua kabisa bei halisi ya bidhaa masokoni.
‘’Kupitia mradi huu wakulima watakwenda kufundishwa kipi kinahitajika sokoni na bei ya mazao yao ni kiasi gani lakini pia wakuma hawa 21,000 tutawaunganisha na masoko ya ndani nan je ya Nchi’’aliongezea.
Sambamba na hayo alisema kupitia mradi huo pia wakulima watafundishwa njia bora za kilimo chai kisichotumia mbolea za kemikali badala yake watatumia mbolea asili zinazoonekana kukosa madhara ya kiafya kinyume na mbolea zinazotumia kemikali.
Hata hivyo afisa huyo aliwataka wanufaika wa mradi huo kujitokeza kwa wingi mara watakapopatiwa taarifa za usajili kwa wakuma kupitia shehia zao na kwamba wasiwe tayari kuipoteza fursa hio adhimu dhidi yao.
Miongoni mwa wanaufaika wa mradi huo kutoka Mkoa wa kusini Unguja ni wananchi wa shehia ya Mtende,shehia ya Muyuni B na Muyuni C.