***********************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba imefanikiwa kutinga fainali katika michuano ya Mapinduzi Cup baada ya kufanikiwa kuichapa Namungo Fc mabao 2-1 kwenye hatua ya nusu fainali .
Magoli ya Simba yaliwekwa kimyani na Mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 7 na goli la pili likifungwa na Miraji Athumani dakika ya 41 ya mchezo.
Goli pekee la Namungo limefungwa na Sey dakika 83.
Simba itakutana na Yanga fainali hapo tarehe 13 kesho kutwa