*************************************
Serikali inatarajia kutoa Mafunzo kwa Walimu wa Vyuo vya Ualimu visivyo vya Serikali.
Hayo yamesemwa Leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo alipokua anafungua Mafunzo ya Wakufunzi yajulikanayo Kama “Teacher Educators Program” TEP yanayofanyika mjini Tabora katika Chuo Cha Ualimu Tabora.
Katika ufunguzi wa Mafunzo haya ya awamu ya Pili Dkt.Akwilapo amesema Wizara kwa kupitia TET imeishatoa Mafunzo hayo kwa Wakufunzi wapatao 707 kutoka Vyuo 28 vya Ualimu.
Amesema, katika awamu ya Tatu ya Mafunzo haya inayotarajiwa kufanyika mapema jumla ya Wakufunzi 190 kutoka Kanda ya kaskazini wanatarajiwa kupatiwa Mafunzo haya sambamba na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Ualimu visivyo vya Serikali.
Amesema Elimu Bora inaanza na mwalimu bora,hivyo Wakufunzi Ni lazima wapatiwe Mafunzo ili kuboresha ujunzi wa ufundishaji.
Amesema,lengo la Mafunzo hayo Ni kuwawezesha Wakufunzi kuongeza umahiri na kukuza taaluma katika kutekeleza majukumu yake ya ufundishaji.
Aidha,amewataka Wakufunzi hao kuhakikisha wanatumia Mafunzo hayo kuleta matokeo chanya katika utendaji wa kazi.”mhakikishe viwango vya wahitimu katika ufaulu vipo katika viwango vya juu, na iwe Ni aibu kwa Chuo kuwa na wahitimu wenye ufaulu duni”. Amesema
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt Aneth Komba amesema, mafunzo hayo yanaratibiwa na TET kwa kushirikiana na kitengo Cha Ualimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Amesema,TET iliendesha Mafunzo hayo kwa Awamu ya kwanza Mwezi juni 2020 ambapo jumla ya washiriki 415 walipata Mafunzo.
Mafunzo ya awamu ya Pili yanawashiriki 292.
Amesema Mafunzo yanalenga kukuza taaluma na utaalamu wa mkufunzi katika kutekeleza mitaala ya Mafunzo ya Ualimu tarajali ngazi ya Astashahada na Stashahada , ambapo taaluma ya Elimu ya Ualimu inatiliwa mkazo katika uandaaji wa mwalimu tarajali.
Ameeleza kuwa ,mafunzo yanatolewa katika maeneo sita ambayo yatamsaidia mkufunzi kujenga umahiri katika ufundishaji na usimamizi wa Mambo ya Elimu kwa ujumla.