Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule 17 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, walipowakutanisha katika kambi la siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma kwa lengo la kuwafundisha masuala ya VVU na UKIMWI, Stadi za maisha na mabadiliko ya tabia pamoja na masomo ya sayansi yanavyoathiri maisha ya kila siku.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Gerald Mweli akieleza umuhimu wa kuelimisha watoto wa kike kwa wanafunzi wa kidato cha II, III na IV kutoka shule za Wilaya ya Bahi wakati wa kongamano hilo.
Mkuu wa shule ya Dodoma Sekondari Mwl. Amani Mfaume akizungumza kuhusu taratibu na sheria za shule yake kwa wanafunzi hao wawapo katika kambi hilo ili kuwa na mazingira rafiki ya kujifunza.
Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Bw. Jumanne Isango akizungumza kuhusu masuala ya tahadhari za kuchukua kuepuka maambukizi ya VVU kwa wasichana wakati wa kongamano hilo.
Afisa Elimi Wilaya ya Bahi Bi. Hellen Msellem akitoa salamu kwa wanafunzi hao, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kongamano hilo wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya vipindi kuanza rasmi.
Sehemu ya wanafunzi hao wakiendelea na michezo mbalimbali wakati wa vipindi vya stadi za maisha, waliopo katika kambi maalumu katika shule ya sekondari ya Dodoma.
Baadhi ya walimu na wawezeshaji wa wanafunzi wa kongamano hilo wakiwa kwenye michezo mara baada ya kumaliza vipindi vya jioni.
Wanafunzi walioshiriki mafunzo ya masuala ya UKIMWI na stadi za maisha wakimsikiliza kocha wao wakati wa maandalzi ya michezo kwa ajili ya kulinda afya zao na kujiweka tayari kwa masomo ya jioni.Wanafunzi hao ni wanaotoka katika Kaya masikini wanaosaidiwa na TACAIDS kupitia mradi wa Timiza ndoto yako kutoka Shule 17 za Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na wanafunzi hao, waliokutana katika shule ya Dodoma Sekondari na kuweka kambi la siku tano kuanzia januari 3 hadi 8, 2021kwa ajili ya kujifunza stadi za maisha na elimu kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)