Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakishusha mizingo katika kituo cha cha Miyuji kilichopo Dodoma walipotembelea na kutoa misaada ya vitu mbalimbali venye thamani ya shilingi milioni tano.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akiteta jambo na watoto wanaolelewa katika kituo cha Miyuji mara baada ya kutembelea na kutoa misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akigawa misaada mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Miyuji baadhi ya watumishi wa REA wametembelea kituo hicho na kutoa misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akimkabidhi Mbuzi Sister Aurea Kyara katika kituo cha Miyuji mara baada ya kutembelea na kutoa misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kituo cha Miyuji mara baada ya kutembelea kituo hicho na kutoa misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akimkabidhi Sister Aurea Kyara kiasi cha milioni moja kwa ajili ya mahitaji kwa watoto katika kituo cha Miyuji mara baada ya kutembelea kituo hicho na kutoa misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Baadhi ya vijana wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Rahman Orphanage Center wakipokea misaada ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na REA.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akizungumza na watoto wanolelewa katika Kituo cha Yatima cha Rahman Orphanage Center mara baada ya kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akimkabidhi kiasi cha shilingi milioni moja Msaidizi wa Kituo cha Yatima cha Rahman Orphanage Center Bi.Aisha Mohamed mara baada ya kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akiwakabidhi watoto misaada ya vitu mbalimbali walivyovitoa katika Kituo cha Yatima cha Rahman Orphanage Center yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Rahman Orphanage Center mara baada ya kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni tano leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Menejimenti na Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA), wametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya Sh.Milioni 10 katika vituo viwili vya kulelea watoto yatima na wenye ulemavu Jijini Dodoma kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya mwaka mpya 2021.
Vituo vilivyopatiwa misaada hiyo ni pamoja na Kituo cha Miyuji na Kituo cha Yatima cha Rahman.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa REA, wakati wa kukabidhi misaada hiyo kwenye vituo hivyo, Afisa uhusiano wa REA, Jaina Msuya amesema wametoa misaada hiyo ili watoto hao washerehekee sikukuu hiyo kama watoto wengine.
Amesema miongoni mwa vitu walivyovitoa ni vyakula, Vinywaji,Mbuzi na vifaa vya shule vya wanafunzi ikiwamo madaftari na peni ili viweze kuwasaidia kipindi shule zitakapofunguliwa mwezi wa kwanza 2021.
” Tumeamua kutoa misaada hii ikiwa ni kuonesha kuwa tunawathamini hawa watoto pia nao washerekee sikukuu ya mwaka mpya vizuri, tumetoa vyakula vinywaji na haya madaftari yawasaidie watoto shule zitakapofunguliwa,” amesema Msuya
Mbali na misaada hiyo pia wametolewa kiasi cha Sh.Milioni 1.2 kwa kila kituo ili fedha hizo zitumike kununua mahitaji mengine.
Aidha amesema REA wataendelea kushirikiana na vituo ili watoto hao wapate faraja na kujiona ni miongoni mwa jamii.
Hata hivyo Msuya amewahimiza watu binafsi, Mashirika na taasisi mbalimbali kuona haja ya kusaidia vituo kama hivyo ambavyo vinalea watoto yatima na wenye ulemavu.
Akitoa Shukrani, Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wenye ulemavu cha Miyuji, Sister Aurea Kyara ameishukuru REA kwa misaada hiyo na kubainisha kuwa itakwenda kusaidia katika malezi ya watoto na watafarijika.
Sister Aurea amewahimiza wadau wengine kujitokeza kuwasaidia watoto na kuona jukumu hilo ni lao ili watoto wapate upendo na faraja.
Naye, Msaidizi wa kituo cha Rahman Orphanage Centre Aisha Mohamed,ameshukuru REA kwa msaada wao walioutoa na kwamba wanawaombea Mungu awabariki kwa kile walichotoa kwa watoto hao.