Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wafanyakazi wa Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge nchini (MKURABITA) alipowatembelea katika ofisi zao viwanja vya nane nane nzuguni Dodoma ili kujitambulisha na kujua majukumu yao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiteta jambo na Mratibu wa Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge nchini (MKURABITA) Dkt.Seraphia Mgembe wakati alipowatembelea katika ofisi zao viwanja vya nane nane nzuguni Dodoma ili kujitambulisha na kujua majukumu yao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge nchini (MKURABITA) mara baada ya kuzungumza nao.
Watumishi wa Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge nchini (MKURABITA) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi(hayupo pichani) wakati alipowatembelea katika ofisi zao zilizopo viwanja vya nane nane nzuguni Dodoma ili kujitambulisha na kujua majukumu yao.
Mkurugenzi wa Idara ya waasisi wa Taifa Bw.Salum Kyando akielezea utendaji kazi wa Idara hiyo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi(kulia kwake) wakati alipotembelea ofisi hizo kwa lengo la kujitambulisha na kujua majukumu yao
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO