Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, Pierre Canton Bacara (katikati), Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini, Bw. Joseph Mutalemwa (kushoto), na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Bi. Mwangaza Matotola, wakibonyeza kitufe kuzindua kampeni ya msimu wa sikukuu ya ‘Magifti ya Viwango’ kwa wakazi wa Kanda ya nyanda za juu kusini katika hafla iliyofanyika jijini Mbeya jana. Ndani ya kipindi cha miezi mitatu ijayo, wateja wa Nyanda za Juu Kusini na Tanzania nzima kwa ujumla watajishindia Sh.milioni 1 kila siku, iPhone 18 mpya kila wiki, Sh milioni 10 kila mwezi, pamoja na zawadi kuu ya gari lenye thamani ya Sh milioni 100.

…………….

*Gari jipya aina ya Jetour lenye thamani ya Sh milioni 100 ni zawadi kuu.

*Zawadi nyingine ni Sh milioni moja kila siku, iPhone 18 kila wiki na Sh milioni 10 kila mwezi.

Mbeya, 25 Novemba 2026. Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania imezindua kampeni yake ya sikukuu ya ‘Magifti ya Viwango’ kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika hafla iliyofanyika leo jijini Mbeya. Hafla hiyo imefanyika takribani wiki moja tu baada ya uzinduzi rasmi wa kitaifa uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, Pierre Canton Bacara, alisema kampuni hiyo imepeleka kampeni hiyo Mbeya ili kuwashukuru wateja katika maeneo wanayoishi na kufanyia biashara.

“Hii ni njia yetu ya kuwashukuru wateja wetu wanaopatikana maeneo mbalimbali na sio kwa wateja wa Dar es Salaam pekee,” alisema Bacara.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Yas Tanzania, Mwangaza Matotola, alisema kampeni hiyo ya miezi mitatu iko wazi kwa wateja wote wa Yas nchini. Alisema wateja wanaweza kuingia kwenye droo wanapotumia huduma za kawaida za kampuni bila kulipa ada ya aina yoyote ili kushiriki.

“Kwanza pakua Yas App na ujisajili. Ukifanya hivyo tu, unakuwa umejiweka katika nafasi ya kuingia kwenye droo papo hapo,” alisema Matotola.

Alifafanua kuwa kila kifurushi cha siku, wiki au mwezi anachonunua mteja kupitia Yas App au menyu ya *147*00# au huduma ya Yas Rusha kinampa nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye droo. Wateja wanaolipia bili za intaneti ya faiba au kufanya marejesho ya mikopo ya simu na rauta nao wanaingia kwenye droo moja kwa moja.

Matotola aliwakumbusha wateja kuwa Yas itawapigia simu washindi kupitia namba rasmi 100 pekee na kwamba hawatahitajika kulipa fedha zozote ili kupokea zawadi zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kusini, Bw. Joseph Mutalemwa, alisema wakulima, wafanyabiashara na wachimbaji madini ni miongoni mwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini wanaotegemea huduma za mawasiliano katika shughuli zao.

“Mbeya ni kitovu cha kilimo, biashara na usafirishaji wa mipakani. Wakulima, wafanyabiashara na wamiliki wa biashara ndogo hapa wanatumia mtandao wetu kila siku kufikia masoko, kupokea malipo na kuendesha shughuli zao za kila siku,” alisema Mutalemwa.

Kampeni hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya ‘Mwaka wa Viwango’. Kwa mujibu wa Yas, kampuni hiyo imewekeza zaidi ya Sh trilioni 1.2 mwaka huu kuboresha mtandao wake nchini, ikiwemo kupanua huduma za 4G na 5G pamoja na huduma ya kupiga simu kupitia mtandao wa