Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 25 Novemba 2026, anafungua Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 56 wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST), unaofanyika katika Ukumbi wa Kwatunza Beach Jijini Mwanza.
Mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Mabadiliko ya Kizazi: Kujenga Uwezo wa Mfamasia Kuongoza Mageuzi katika Afya na Utengenezaji wa Dawa nchini Tanzania” unawakutanisha wafamasia, wafamasia wasaidizi na wadau wa sekta ya Afya kwa siku tatu, kwa lengo la kubadilisha uzoefu, kujadili maendeleo ya usimamizi wa afya nchini pamoja na kuunga mkono Dira ya Taifa 2050.

