Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, ameshiriki vikao vya Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, vilivyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kimelenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa majukumu ya Chama Cha Mapinduzi mkoani humo.
Alipowasili, Mhe. Ndejembi amepokelewa na Viongozi na Wanachama wa CCM mkoani humo, ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki vikao hivyo tangu alipoteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mlezi wa Mkoa huo.
Aidha mapokezi hayo yameenda sambamba na gwaride rasmi la vijana wa UVCCM na baadaye kuvikwa skafu maalumu inayoashiria amani, umoja na uwajibikaji.

