Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka katika kuunga juhudi za serikali kuwakomboa vijana ameamua kutoa viti 100 kwa ajili ya kuanzisha mradi kwa umoja wa vijana wa (UVCCM) kata ya Viziwaziwa ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Mhe.Koka mbali na kutoa sapoti kwa kuchangia viti hivyo ameeza kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika kuanzisha mradi wao wa maegesho ya bodaboda ambayo yatakuwa ni fursa ya kuwaingizia kipato.
Koka amechangia msaada huo wakati wa kikao cha baraza la UVCCM Kata ya viziwaziwa ambapo pia amepata fursa ya kufungua rasmi shina la umoja wa vijana bodaboda mkomgeni na kuwataka kuwa na umoja katika kuitunza na kuidhamini miradi ambayo wanaianzisha.
Aidha Mbunge huyo amewaasa vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya fedha kwa ajili ya kuweza kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wao wa mtu mmoja mmoja pamoja na vikundi vyao viwe endelevu.
“Kitu kikubwa ambacho ninawaomba vijana wa UVCCM kata ya viziwaziwa ni kuendelea kushikamana pamoja na kuwa na nidhamu katika suala zima la utunzaji wa fedha ikiwa sambamba na kuifanya miradi walioianzisha kuwa na tija,”amebainisha Mbunge Koka
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Kata ya viziwaziwa Jumanne Mwagiya amempongeza kwa dhati Mbunge koka kwa kuweza kuwashika mkono na kuwasapoti fedha na viti.
Amebainisha kwamba sapoti na msaada ambao wamepatiwa na Mbunge Koka utaweza kuwasadia vijana wa Kata ya viziwaziwa kuweza kuwakomboa katika kujikwamua kiuchumi na kuleta chachu ya maendeleo.
Naye Diwani wa Kata ya vizjwaziwa Mhe.Mohamed Chamba amebainisha kwamba juhudi ambazo zimefanya na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge Koka zimeweza kuleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali.
Nao baadhi ya vijana wa UVCCM kata ya viziwaziwa ambao wameshiriki katika kikao hicho cha baraza hawakusita kumpongeza Mbunge wao kwa kuwashika mkono katika suala la kuwasaidia milioni moja ili kuanzisha mradi wa maegesho ya pikipiki pamoja na mradi wa viti 100.

