Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, ametembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha mabasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, mkoani Lindi, akisisitiza mradi huo uwe chachu ya ajira, biashara na ongezeko la mapato kwa manufaa ya wananchi.
Akizungumza na wananchi, ameelekeza kujengwa kwa mzunguko wa barabara katika makutano muhimu ya Mtama na kuandaliwa kwa mafunzo yatakayowawezesha vijana wa Lindi na Mtwara kunufaika na fursa za mradi wa gesi ya LNG.
Aidha, amewataka viongozi kuchukua hatua dhidi ya wanaochochea migogoro ya wakulima na wafugaji, ili wananchi waendelee na shughuli zao kwa amani.
Makamu wa Rais yuko mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi, akikagua miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

