Viongozi wa Serikali wametakiwa kuwashirikisha wananchi katika ulinzi na uendelezaji wa vyanzo vya maji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) amesema hayo wilayani Kilombero leo Novemba 8, 2026.
Mhe. Kiswaga akiongoza kamati huyo katika ziara ya kikazi kukagua utetekelezaji wa miradi ya maji ameainisha kuwa utunzaji wa vyanzo vya maji ni lazima kwa uendelevu wa miradi ya maji na maisha ya sasa na baadae.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya akiipokea kamati hiyo ofisini kwake amesema Serikali inapokea maelekezo ya kamati na inafanya kazi saa 24 kulinda mazingira na kutoa suluhu kwa changamoto zunazoibuka ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Amesema uwepo wa kamati katika wilaya ya Kilombero ni fursa ya kufanya vizuri zaidi katika utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji.

