Na Victor Masangu, Pwani 
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wametakiwa kuachana kabisa  na vitendo vya kuwa na  makundi, magonvi na mivutano hali ambayo  inayoweza kusababisha kubomoa misingi imara  iliyoachwa na waasisi  waliotangulia. 
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa pili wa Rais wa  Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Hayo yamesemwa wakati akiwahutubia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere uliopo eneo la kwa mfipa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
Makamu huyo wa pili wa Rais pia ndiye mlezi mpya wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani ambapo pia ameahidi kushirikiana na viongozi na wanachama wa CCM katika kukijenga chama pasipo kuwa na makundi.
“Chama chetu ni chama ambacho ndio kipo madarakani na kinapendwa sana na wananchi lakini hakiwezi kujengwa kwa makundi,makundi,wala mvutano, amebainisha Mhe. Abdulla 
Amesema hakuja Pwani kulea makundi bali amekuja kulea kundi la Chama Cha Mapinduzi. 
Pia ameendelea kusema kwamba viongozi wote lazima wafanye kazi kama timu katika kukisimamia Chama Cha Mapinduzi kwa kufuata Katiba, Kanuni na Miongozo mbali mbali ambayo ipo.
 Makamu huyo wa Pili wa Rais amesema kwamba  hakuna sababu yoyote ile ya kuvutana kwani kwa kufanya hivyo sawa na sumu itakayokiumiza Chama Cha Mapinduzi. 
Katika hatua nyigine mempongeza amempongeza  kwa dhati Rais wa awamu ya  sita Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kurejesha heshima ya Chama Cha Mapinduzi na kuwafanya Watanzania kuwa na hali ya amani na utulivu kwa  Serikali yao.
Nao baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi  CCM Mkoa wa Pwani wameahidi kumpa ushiriķiano mkubwa wa hali na mali mlezi wao ikiwa pamoja na kuyafanyia kazi maelekezo yote ambayo ameyatoa  kwa ajili ya maslahi mapana ya chama