Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, (kushoto), akimkaribisha Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi,  baada ya kuwasili kwenye ofisi za wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, (kulia), akiagana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika kwenye ofisi za wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akizungumza wakati wa kikao na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), (hayupo pichani), kilichofanyika katika ofisi za wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, akizungumza wakati wa kikao na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, kilichofanyika katika ofisi za wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma. Kwa upande wa ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Joshua Nsubili
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua (katikati), Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Bw. Rished Bade (kulia) na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedek Mbise, wakisikiliza maelezo ya Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, (hayupo pichani), wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ofisi za wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma
Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Bw. Rished Bade, akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ofisi za wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, (wa tatu kutoka kulia) na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na JICA, baada ya kumalizika kwa kikao chao, kilichofanyika kwenye ofisi za wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma. (Picha na Kitengo Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

…………..

Na. Farida Ramadhan na Josephine Majura, WF, Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeialika Serikali ya Japan pamoja na sekta binafsi ya nchi hiyo kushiriki katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Dira 2050) kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali za kipaumbele zilizobainishwa katika dira hiyo.
Wito huo ulitolewa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo, Bw. Hiroyuki Kobayashi.
Bw. Joshua alisema kuwa Dira 2050 imeweka mfumo wa ushiriki wa sekta binafsi na ya umma katika kugharamia na kutekeleza miradi ya maendeleo, ambapo sekta binafsi inatarajiwa kuchangia asilimia 70 na sekta ya umma asilimia 30.
Alisema Tanzania imeikaribisha Japan kuunga mkono Serikali katika kutekeleza wajibu wake wa kuchangia asilimia 30 ya rasilimali zinazohitajika, sambamba na kuhamasisha sekta binafsi ya Japan kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali ya kipaumbele yaliyoainishwa kwenye Dira 2050.
Aidha, alisema kuwa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaanza kutekeleza ajenda mpya ya maendeleo kupitia Dira 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV), Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na Japan ili kufanikisha malengo ya maendeleo ya muda mrefu.
Aliongeza kuwa katika mazungumzo hayo, pande hizo zilijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano, yakiwemo utekelezaji wa miradi ya barabara na kuimarisha usalama wa chakula.
Bw. Joshua aliishukuru Serikali ya Japan na JICA kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa muda mrefu, hususan katika kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa JICA, Bw. Hiroyuki Kobayashi, aliipongeza Tanzania kwa kuandaa Dira 2050 yenye malengo makubwa na mwelekeo ulio wazi wa maendeleo ya nchi.
Alisema JICA iko tayari kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania ili kusaidia utekelezaji wa dira hiyo, kuongeza mapato na kuvutia uwekezaji.