Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Thabit Kombo alikisalimiana na Mfalme Charles III wa Tatu na Waziri Mkuu wa Uingereza Mheshimiwa Andy Burnham.
………
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, akimwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa Viongozi na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola na Watendaji Wakuu wa Makampuni uliofanyika Kisiwani Antigua, nchini Antigua na Barbuda.
Pembezoni mwa mkutano huo, Mhe. Waziri Kombo alikutana na Mfalme Charles III wa Tatu; Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa Andy Burnham; Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda, Mheshimiwa Gaston Browne na Gavana Jenerali wa Visiwa hivyo Mhe. Sir Rodney Williams.
Mkutano huo wa CHOGM unawakutanisha viongozi wote hao pamoja na wa serikali za nchi wanachama wote na wa sekta binafsi kujadili fursa za kuhamasisha uwekezaji, kuimarisha ustahimilivu wa uchumi na kuongeza ajira katika nchi za Jumuiya ya Madola.
Majadiliano yalihusu miundombinu, nishati jadidifu, kilimo na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, huku yakisisitiza ushirikiano wa vitendo kati ya serikali na wawekezaji hao pamoja na ushirikishwaji mkubwa zaidi wa Sekta Binafsi kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.
Ushiriki wa Tanzania ulitoa fursa muhimu ya kuimarisha mahusiano ya kimataifa na kuendeleza diplomasia ya uchumi kwa ajili ya kuvutia uwekezaji na kukuza ustawi wa pamoja na kuelezea Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi kupitia Dira 2050.

