Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi amezindua rasmi mbio za Musoma Marathon, ambazo zinatarajiwa kuanza Disemba 18-20 mwaka huu zikihusisha michezo mbalimbali ambazo zinamalengo yakwenda kusaidia ukamilishaji wa vyumba vya madarasa.
Akishirki katika zoezi hilo asubuhi yaleo Brigedia jenerali Evans Mtambi anahapa anawataka wana mara na wananchi wa mikoa mingine kushiriki kikamilifu katika katika mbio hizo ambazo zitafanyika Rasm Disemba 18-20 mwaka huu.
Akizungumza katika uzinduzi wa marathon hiyo mwenyekiti wa Musoma Marathon Suzana Senso alisema wameandaa mbio hizo ambazo zinalengo kwenda kuchangia upauaji wa vyumba vya madaraka katika mkoa wa Mara katika shule za sekondari ikiwa nalengo la kupokea wanafunzi wa kidao cha kwanza mwakani 2027.
Suzana amesema mbio hizo zitafanyika rasmi Disemba 18-20 huku mshindi wa kwanza wa km 21 atapewa kitita cha shilingi Milioni 1.5,mshindi wa pili akipokea shilingi milinon 1.2 watatu milioni 1 na mshindi wanne laki 7 watano laki 5 na washindi wengine hadi wakumi nao watapatiwa zawadi.

