Kamati ya Ushauri wa Kisheria Mkoa wa Iringa, imefanya kikao chake cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, zilizopo katika Jengo la NSSF Akiba House, Iringa tarehe 29 Oktoba, 2026.
Wakili wa Serikali Mkoa wa Iringa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, *Bi. Radhia Njovu* ameongoza kikao hicho kilicholenga kujadili majukumu ya Kamati ya Ushauri wa Kisheria ya Mkoa, pamoja na kuweka maazimio na vipaumbele vya utekelezaji wa shughuli za kamati kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uratibu na ushirikiano wa kisheria katika ngazi ya mkoa, kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kamati na kuhakikisha utoaji wa huduma za ushauri wa kisheria unazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
