Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa 15 de Agosto mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa leo, Oktoba 25, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC katika mchezo huo yamefungwa na Anicet Oura, Elie Mpanzu na Keletso Makgalwa.

Kwa matokeo hayo, Simba SC wamefuzu hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 9-1, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza.