Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka (katikati) akipokea madawati kutoka kwa wadau kupitia Shirika la Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya Shule ya Wenye Mahitaji Maalum Mazinyungu, jana Wilayani Kilosa.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Mhe. Shaka alisema, *”Madawati haya sio mbao na misumari tu. Madawati haya ni ndoto ya watoto wetu wenye uhitaji kutimia, leo wadau hawa wametuletea maji jangwani.”