Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Dodoma 

Wakala wa Vipimo (WMA) umefanya ukaguzi wa vipimo 5,015 katika mwaka wa fedha 2025/2026, sawa na kuvuka lengo lililowekwa kwa asilimia 25.

Akizungumza Septemba 18, 2026 jijini Dodoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, amesema WMA Ilipanga kufanya ukaguzi wa vipimo 4,000 katika kipindi hicho.

 Amesema kuwa ukaguzi huo unalenga kuhakikisha vifaa vya vipimo vilivyokwisha hakikiwa vinaendelea kutumika kwa usahihi.

Amesema ukaguzi pia unalenga kubaini iwapo kuna mabadiliko au udanganyifu katika matumizi ya vifaa hivyo baada ya kuhakikiwa.

Amebainisha kuwa ukaguzi huo hufanyika kwa mipango maalumu lakini pia unaweza kufanyika baada ya WMA kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi.

Ameongeza Kuwa hatua hiyo inalenga kulinda maslahi ya mtumiaji wa huduma pamoja na mtoa huduma.

Aidha, amesema WMA ilikagua bidhaa za ndani 21,262 katika kipindi hicho.

Ameongeza kuwa bidhaa zilizoingizwa nchini kupitia mipaka na bandari zilizokaguliwa zilifikia 17,774.

ukaguzi huo ni sehemu ya kuhakikisha bidhaa zinazouzwa kwa vipimo zinakidhi masharti yaliyowekwa.

Amesema WMA itaendelea kufanya ukaguzi ili kuhakikisha vipimo na bidhaa zinazouzwa kwa vipimo vinakuwa sahihi na vinamlinda mlaji.