Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeonya wananchi kuhusu uwepo wa chanjo bandia ya mifugo aina ya TMEVAC NDV Strain 1-2 inayosambazwa nchini.

TMDA imesema chanjo hiyo haikuzalishwa na Tanzania Veterinary Laboratory Agency (TVLA), huku ikibainisha kuwa ina tofauti kadhaa na chanjo halisi, ikiwemo maandishi kwenye lebo na namba ya toleo.

Mamlaka imewataka wafugaji na wamiliki wa kliniki za mifugo kuwa waangalifu, kutonunua chanjo hiyo na kutoa taarifa kwa TMDA kupitia 0800110084 au [email protected].