Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza kikao cha Baraza la Taifa la Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, kilichofanyika leo, tarehe 12 Septemba 2026, Ikulu Zanzibar.
Kikao hicho kimewakutanisha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mawaziri kutoka Wizara mbalimbali, pamoja na viongozi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Kikao hicho kimelenga kujadili na kuimarisha mikakati ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar.

