Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali (Mst) Hamis Rajab Semfuko ametembelea hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kujengwa katika eneo hilo, Septemba 10, 2026 Jijini Arusha.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Semfuko amesisitiza usimamizi makini wa miradi inayotekelezwa kwa kuzingatia viwango vyenye ubora na kukamilishwa kwa wakati ili kuepusha ucheleweshaji wa miradi na kuongeza ufanisi wa matumizi ya fedha.
“ ujenzi umefanyika vizuri na kwa mwendo wa haraka pamoja na kwamba eneo ni jipya lakini tayari pameanza kupata watalii wengi kutoka maeneo tofauti tofauti huku makampuni mengi ya utalii yakionesha nia ya kuleta watalii zaidi. “ amesema Semfuko
Aidha, Semfuko amesema kuwa hifadhi ya Makuyuni ni tegemeo kubwa kwa watalii wa picha katika ukanda wa kasikazini na kwamba bodi ya TAWA itahakikisha mradi wa Public Campsite, Animal hideout, Picnic site na lango kuu la kuingia hifadhini linapewa kipaumbele na kukamilika kwa wakati ikiwa ni mapango mkakati wa kupokea watalii wengi kuelekea mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mnamo mwaka 2027.
“ Nimefurahishwa na maendeleo ya miradi yote, hatua ni nzuri sana jambo ambalo linazidi kuvutia watalii wa ndani na nje kutokana na mwonekano mpya uliopo hivi sasa katika hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park. “ amesema Semfuko

