Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa heshima za mwisho kwa Marehemu Hafidh Ameir Hassan, mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mazishi yaliyofanyika leo, tarehe 07 Septemba 2026, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, viongozi wa dini, pamoja na familia, ndugu, jamaa na wananchi.

Mapema, Rais Dkt. Mwinyi ameungana na familia, ndugu na jamaa katika Sala ya Jeneza iliyofanyika Masjid Ihtiswam, Kizimkazi, kabla ya mwili wa Marehemu Hafidh Ameir Hassan kuzikwa katika makaburi maalum ya Kizimkazi.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa mkono wa pole kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, watoto na familia ya Marehemu, na kuwafariji katika kipindi hiki cha majonzi.

Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.