Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, akiongoza kikao cha utatuzi wa mgogoro wa haki madini na haki ardhi baina ya Kampuni ya Barrick na wachimbaji wadogo wa madini wa Tarime,Mkoani Mara.

Kikao hicho cha maridhiano, kimefanyika leo tarehe 4 Septemba, 2026, jijini Dodoma ambapo Waziri Mavunde amezitaka pande zote mbili kukaa na kujadiliana ili kuangalia namna ya bora ya kufika muafaka kwa kuzingatia maelekezo ya Sheria ya Madini Sura 123.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya Tarime, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Katibu Tawala Wilaya ya Tarime, Wawakilishi wa mgodi wa North Mara na walalamikaji.