Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kubadilishana uzoefu kufuatia agizo la Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzitaka taasisi za afya kujifunza kutoka kwa wenzao na kuboresha huduma za afya nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kubadilishana uzoefu kufuatia agizo la Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzitaka taasisi za afya kujifunza kutoka kwa wenzao na kuboresha huduma za afya nchini.

Mtaalamu wa Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Chuvaka akiwaelezea namna maabara ya kisasa inayotumia teknolojia ya roboti na akili unde (AI) inavyofanya kazi viongozi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kubadilishana uzoefu kufuatia agizo la Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzitaka taasisi za afya kujifunza kutoka kwa wenzao na kuboresha huduma za afya nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akizungumza wakati viongozi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kubadilishana uzoefu kufuatia agizo la Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzitaka taasisi za afya kujifunza kutoka kwa wenzao na kuboresha huduma za afya nchini.

Viongozi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wakiwa nje ya chumba cha upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa cathlab walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kubadilishana uzoefu kufuatia agizo la Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzitaka taasisi za afya kujifunza kutoka kwa wenzao na kuboresha huduma za afya nchini

Viongozi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wakifuatilia wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge anazungumza walipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kubadilishana uzoefu kufuatia agizo la Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzitaka taasisi za afya kujifunza kutoka kwa wenzao na kuboresha huduma za afya nchini.

……….

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

 Viongozi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa JKCI ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzitaka taasisi za afya kujifunza kutoka kwa wenzao na kutumia uzoefu huo kuboresha huduma za afya nchini.

 Kupitia ziara hiyo viongozi hao wamepata fursa ya kujifunza namna JKCI inavyotekeleza majukumu yake, hususan katika eneo la huduma kwa wateja na mikakati ya kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora kwa wakati.

 Akizungumza wakati ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema taasisi za afya zinapaswa kujikumbusha mara kwa mara umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wateja na kubuni njia mpya za kuwahudumia wagonjwa.

 “Ni vyema kila mara tukawa tunakumbushana kuhusu namna bora ya kutoa huduma kwa wateja, kwa kufanya hivyo tutawavutia watanzania kupata huduma za matibabu hapa nchini na kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda nje ya nchi kwaajili ya kupata matibabu”, alisema Dkt. Kisenge

 Dkt. Kisenge alisema JKCI imewekeza kwa wataalamu wa huduma kwa wateja, ambao husaidia kuwakaribisha, kuwasikiliza na kuwatuliza wagonjwa pamoja na ndugu wa wagonjwa pale wanapohitaji msaada wa huduma.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya alisema taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi nyingine katika kubadilisha uzoefu lengo likiwa ni kuboresha huduma.

 Dkt. Angela alisema kabla ya wataalamu wa MOI kutembelea JKCI, wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) nao walitembelea JKCI kujifunza kuhusu ufanisi uliopo na kuahidi kwenda kuufanyia kazi.