Leo 01 September 2026, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB) amekutana na wakurugeni wa Kampuni ya Mantra Tanzania Limited mjini Dodoma kujadili maendeleo ya mradi wa mto Mkuju unaojihusisha na uchimbaji wa madini ya urani wilayani Namtumbo,Ruvuma.
Akiongoza ujumbe huo Bw. Vladislav Shulga amesema kuwa kampuni ya Mantra Tanzania Limited ipo tayari kuendelea na ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kipekee Tanzania na Afrika mapema iwezekanavyo ndani mapema Oktoba 2026 mwaka huu baada ya kuzinduliwa mtambo mdogo wa uchakataji wa Urani mwaka jana 2025.
Akizungumza katika mkutano huo,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde ameitaka Kampuninya Mantra kuhakikisha hatua za uendelezaji mradi zinaendelea kwa kasi kubwa na pia ameuhakikishia uongozi wa Mantra Tanzania kuwa wataendelea kupata msaada wa serikali katika kila hatua ili kuhakikisha mradi huu unasonga mbele na kuanza uzalishaji ifikapo 2029.
Pichani ni Meneja Uendelevu wa kampuni ya Mantra Bw. Majani Moremi Wambura, kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Bw Vladislav Shulga, na Mjumbe wa Bodi hiyo Bw. Aleksandr Ryabchenko

