Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa- (SUKI) *Ndugu Rabia Abdalla Hamid(MCC)* amewasisitiza wananchi wa mkoa wa Pwani kuendelea kulinda amani na utulivu wa nchi yetu kwani CCM itaendelea kuboresha na kustawisha maisha ya kila mtanzania, kila mtanzania ni sehemu ya historia ya nchi yetu ya Tanzania na kila mtanzania anapaswa kuilinda Tanzania.
Ndg Rabia ameyasema hayo leo tarehe 23/08/2026 katika muendelezo wa ziara yake ya Kusikiliza makundi ya kijamii , kutatua changamoto na kuzungumza nao wakiwamo Viongozi wa Dini, Wazee, Wakulima mbalimbali, wafugaji, NGO’s, Umoja wa Wasusi, Wafanyabiashara, wanamichezo mbalimbali, wavuvi, wanavyuo, waalimu, Machinga, Mawinga, Mama Lishe, Baba Lishe, vyama vya ushirika, Umoja wa mashamba ya chumvi, Wajane, wachimbaji wa madini, Maafisa Usafirishaji na vikundi mbalimbali vya Ujasiliamali.

