Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi na viongozi wengine wakati alipowasili katika eneo la Mradi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP).
Rais Samia atazindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 leo tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.

