Katika picha wa kwanza kulia ni Meneja wa VETA Kanda ya Kaskazini Monica Mbella, akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya ufundi stadi kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan jinsi yanavyonufaisha makundi mbalimbali katika jamii alipotembelea banda la VETA katika Tamasha la Kizimkazi linalofanyika katika viwanja vya Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar. 

Tamasha hilo lenye kaulimbiu Kizimkazi kumenoga, shangwe na fursa limezinduliwa leo tarehe 12 Agasti, 2026 na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ally Mwinyi na linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 14 Agasti, 2026.