Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ambayo anatarajia kuifanya kuanzia leo Julai 20,2026.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya ziara ya kikazi ambayo anatarajia kuifanya mkoani humo kuanzia leo Julai 20,2026.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ambayo anatarajia kuifanya kuanzia leo Julai 20,2026.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John, wakati akiwa Mkoani Pwani kwa ajili ya ziara ya kikazi, Julai 20,2026.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule Forest ambay0 ni mchepuo wa Kiingereza katika Kata ya Kongwe Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wakati akiwa mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi, Julai 20,2026.

……………. 

Na; Mwandishi WetuKibahaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewataka wawekezaji katika sekta ya viwanda kuzingatia uwekezaji unaofuata taratibu na sheria ya Mazingira.

Masauni amesema hayuko tayari kufanya ziara kwa ajili ya kufunga Viwanda vilivyokiuka sheria za Mazingira ambavyo vingekuwa kimbilio kwa vijana na kupunguza tatizo la ajira.

Masauni ameyasema hayo Julai 20, 2026 alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Pwani katika Wilaya ya Kibaha na kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kuweka jiwe la Msingi kwenye kituo cha biashara kilichojengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule mpya ya mchepuo wa Kiingereza katika Kata ya Kongwe.

“Tunahitaji uwekezaji huu kwa ajili ya watoto wetu hatupendi uwekezaji usiofuata sheria ya mazingira, tuendelee kuhakikisha tunawasiliana na mamlaka za mazingira uwekezaji huu usiwe kero kwa wananchi,” amesema Mhe. Masauni amesema ni muhimu kila mmoja atimize wajibu wake anapofanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini iwe faida kwa jamii.

Vijana hawapaswi kuwa watazamaji kwenye uwekezaji uliofanyika Kibaha, ili Wawekezaji walipe kodi watahitaji vijana wanaofanya kazi ndio maana Serikali ikaamua kujenga vituo hivyo kuwaandaa vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.Amesema Mkoa wa Pwani umekuwa kiungo cha mkoa wa kibiashara wa Dar es Salam na hivyo uwepo wa karakana hiyo ya kisasa karibu na barabarani kuu itahudumia magari yanayotumia njia hiyo.Kwa upande wake,

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge amesema moja ya sababu ya wawekezaji kuukimbilia na kuwekeza mkoa humo ni uwepo wa umeme wa uhakika tofauti na miaka yanyuma.

“Mkoa wa Pwani tumeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wetu ndio maana kila kukicha kumekuwa na ongezeko la viwanda ambapo imesaidia katika kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa huu na mapato yetu,” amesema Mhe. Kunenge.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mhe. Silvestry Koka amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika ukusanyaji wa kodi jambo ambalo limekuwa na faida kwa Manispaa kwa kutumia fedha kujenga vitega uchumi na kutoa mikopo ya asilimia kumi.

Amesema ujenzi wa vitega uchumi katika Manispaa hiyo utasaidia kuendeleza dira ya 2050 kupitia sekta binafsi na kuinua uchumi katika harakati za kuboresha sekta hiyo.