Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog,Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Paramagamba Kabudi, amesema usafi wa mazingira unapaswa kupewa kipaumbele, hususan katika usimamizi wa madampo na mitaro ya majitaka, ili kulinda afya ya jamii na mazingira.

Ameyasema hayo Julai 2,2026 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Pili la Kitaifa la Wadau wa Mazingira lililoandaliwa na EWURA, sambamba na uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Usafi wa Mazingira unaolenga kuweka mfumo wa pamoja wa kupanga, kutekeleza, kusimamia na kufuatilia utoaji wa huduma za usafi wa mazingira kwa wananchi.

Aidha, amebainisha kuwa utekelezaji wa sera na sheria za mazingira unapaswa kuimarishwa sambamba na juhudi za kulinda vyanzo vya maji, akisisitiza kuwa uwekezaji katika usafi wa mazingira ni msingi muhimu wa kulinda afya za wananchi na kukuza maendeleo ya taifa.

Aidha, ameongeza kuwa miongoni mwa changamoto zinazokwamisha usafi wa mazingira ni athari za mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la makazi yasiyo rasmi, upungufu wa vyoo bora katika masoko na maeneo ya biashara, pamoja na ukosefu wa sehemu maalum za kunawia mikono zenye maji tiririka katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.

Pia, ‎amesema Kuwa majitaka yasipotibiwa na madampo yasiposimamiwa ipasavyo husababisha uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha afya ya binadamu, hivyo amewataka wadau wanaoshiriki kongamano hilo kuja na mikakati ya pamoja ya kuboresha usimamizi wa madampo na miundombinu ya majitaka.

‎Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Fedha kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Stanley  Mahembe  amesema takwimu za tathmini ya utendaji wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira za mwaka 2024/2025 zinaonyesha kuwa kati ya mamlaka 84 za maji na usafi wa mazingira nchini, ni mamlaka 24 pekee zenye miundombinu ya kutibu majitaka