Serikali inaendelea na hatua za awali za ujenzi wa bwawa la Farkwa ambapo Wizara ya Maji kupitia programu ya Uhimilivu dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ( DSRSWSP) inahamisha nyenzo katika maeneo ya umma ikiwemo shule.

Zoezi linafanyika kwa kushirikiana na ofisi za mamlaka za Serikali za Mitaa wilaya ya Chemba, mkoa wa Dodoma.

Nyenzo zinazohamishwa zinatoka shule ya msingi Bubutole na shule ya msingi Mombose na kupelekwa katika shule mpya ya Sankwaleto kuboresha miundombinu.

Kinachoendelea kwa sasa ni kukusanya na kusafirisha.

Zoezi hilo ni endelevu kwa Wizara ya Maji kupitia program ya DSRSWSP na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kuandaa eneo la mradi.

Mradi wa bwawa la Farkwa unafadhiliwa AfDB.