Timu ya Taifa U17 ya Senegal imetwaa ubingwa wa mashindano ya AFCON U17 ikiitandika Serengeti Boys kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Mchezo huo ulienda hadi kwenye changamoto ya mikwaju ya Penalti baada ya kumalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Huu unakuwa ubingwa wa pili kwa Senegal U17 huku Serengeti Boys ikiandika rekodi ya kufika fainali ambapo haikuwa kutokea hapo awali huku ikicheza mechi zote za mashindano bila kupoteza ndani ya dakika 90.