WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amerejea nchini Tanzania akitokea jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo alikomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Dkt. Mwigulu aliagwa na Meya wa Jiji la Brazzaville, Dieudonné Bantsimba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya, Brazzaville Mei 27, 2026.

